Kampuni ya Google imezindua programu yake mpya kwa jina DUO. Programu hiyo ni jibu la Google kwa programu nyengine kama ile ya Apple ya Face Time,Skype ya Microsoft na Facebook messanger.
Programu
hii haina tofauti kubwa na programu nyingine zinazotoa huduma za video,
isipokuwa inakupatia uwezo wa ni nani anayepiga simu hivyo basi kumpatia
mtumiaji fursa ya kuamua iwapo ataipokea simu hiyo au la. Programu hiyo
mpya iliotangazwa mwezi May imezinduliwa kama huduma ya bure kwa simu
zinazotumia Android pamoja na simu za Apple za iPhone.
Simu
zinalindwa na haziwezi kudukuliwa na video hubadilika kulingana na kasi
ya kushika simu inayopigwa. Kama programu ya FaceTime, duo inahitaji
namba ya mtu ya simu kuunganishwa. Huduma nyingine zinahitaji mtumiaji
kuingia katika akaunti zao ili kupata fursa ya kupata huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment