Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

SAMSUN IMEZINDUA TV INAYOWEZA KUTAMBUA UWEPO WAKO



Tecknologia hii imerahisisha zaidi kupuguza Matumizi ya Rimoti. TV Hizi zinaweza kutambua kila uhachokifanya kwa wakati husika pia zina Kamera unaweza zipa amri bila kutumia Rimoti au Kibonyezo. Hii inaonyesha ni namna gani wenzetu wavyozidi piga Hatua za kiteknologia katika nchi zao.........

iPHONE 5S kUZINDULIWA RASM WIKI IJAYO


Kampuni ya Apple ambayo ndiyo watengenezaji wa simu za iPhone wametangaza tarehe 10 mwezi huu kuwa ndiyo siku ambayo wataitambulisha simu mpya ya iPhone 5s rasmi. Simu hii mpya ambayo pia itakuja na cover yenye rangi ya gold ikiongezeka kutoka kwenye rangi nyeusi na nyeupe ambazo zilikuwa ndiyo rangi pekee. Mitandao tofauti ya mambo ya digital imesema kwamba simu hii mpya kunauwezekano mkubwa wa kuja na uwezo wa kutambua fingerprint ya mtumiaji ambayo itatumika kama lock ya simu. Kitu kingine inasemekana siku hiyo pia itazinduliwa rasmi link ya watumiaji wa simu za iPhone ku-update operation system ya simu zao kuwa iOS7.

FACEBOOK YAPANGA KUWASAIDIA WATU MASIKINI WASIO MUDU GHARAMA ZA INTERNET


Mpango wa kuhakikisha internet inawafikia watu wengine bilioni 5 waliosalia duniani umeanzishwa na mwanzilishi wa Facebook , Mark Zuckerberg.
Mtandao huo wa kijamii umeungana na makampuni ya Ericsson, MediaTek, Nokia, Opera, Qualcomm na Samsung, na mengine kupunguza gharama za data.
Kundi hilo limesema linataka watu kwenye nchi zinazoendelea wawe sehemu ya jumuiya ya internet. Zuckerberg alisema lengo ni kuwafikishia internet watu ambao hawawezi kumudu gharama za internet.
Mpaka sasa ni watu bilioni 2.7 tu ndo wenye uwezo wa kupata internet ambayo ni sawa na theluthi ya idadi ya watu duniani.