Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

FACEBOOK YAPANGA KUWASAIDIA WATU MASIKINI WASIO MUDU GHARAMA ZA INTERNET


Mpango wa kuhakikisha internet inawafikia watu wengine bilioni 5 waliosalia duniani umeanzishwa na mwanzilishi wa Facebook , Mark Zuckerberg.
Mtandao huo wa kijamii umeungana na makampuni ya Ericsson, MediaTek, Nokia, Opera, Qualcomm na Samsung, na mengine kupunguza gharama za data.
Kundi hilo limesema linataka watu kwenye nchi zinazoendelea wawe sehemu ya jumuiya ya internet. Zuckerberg alisema lengo ni kuwafikishia internet watu ambao hawawezi kumudu gharama za internet.
Mpaka sasa ni watu bilioni 2.7 tu ndo wenye uwezo wa kupata internet ambayo ni sawa na theluthi ya idadi ya watu duniani.


No comments:

Post a Comment